Msanii wa kufoka wa Canada, K’naan ashtakiwa kwa dhuluma za kingono

Dismas Otuke
1 Min Read

Msanii maarufu wa Canada wa muziki wa kufoka Keinan Abdi Warsame, maarufu kama K’naan wa kibao maarufu cha Wavin’ Flag,ameshtakiwa kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono jijini Quebec miaka 14 iliyopita .

Kulingana na kesi hiyo K’naan alitekeleza uhalifu huo kati ya Juali 16 na 17 mwaka 2010 alipokuwa kwenye tamasha la Quebec city de’ete de Quebec.

Mlalamishi alikuwa na umri wa miaka 29 aliposhambuliwa na mwanamuziki huyo .

Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani Alhamisi wiki jana bila msanii huyo kujitokeza wala mawakili wake .

Share This Article