Msalaba waua padri akiendeleza misa Ecuador

Video ya ibada hiyo ya Jumamosi usiku inaonyesha msalaba mzito uliokuwa ukutani juu ya madhabahu ukimwangukia Padri Sánchez.

Marion Bosire
1 Min Read

Padri wa Kanisa Katoliki aliyekuwa akiendesha Misa ya jioni kusini-magharibi mwa Ecuador amefariki baada ya msalaba kumwangukia wakati wa ibada hiyo iliyokuwa ikirushwa mubashara mtandaoni.

Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Guayaquil, jiji lililoko umbali wa kilomita 265 kusini-magharibi mwa mji mkuu Quito, limemtambua padri huyo kuwa Patricio Sánchez wa Kanisa la Perpetuo Socorro.

Video ya ibada hiyo ya Jumamosi usiku inaonyesha msalaba mzito uliokuwa ukutani juu ya madhabahu ukijitenga na ukuta na kumwangukia Sánchez kichwani alipokuwa akiendesha Misa.

Inaonekana hakuuona msalaba huo ukidondoka.

Waumini walisikika wakipiga kelele za kuomba msaada huku matangazo ya ibada hiyo yakiendelea kwenye mitandao ya kijamii.

Mamlaka za eneo hilo bado hazijatoa maelezo kuhusu tukio hilo.

Sánchez alikuwa mwanachama wa Shirika la Kipadri la Most Holy Redeemer, shirika la kidini la Kanisa Katoliki lililoanzishwa mwaka 1732 na lenye uwepo katika nchi 80 duniani.

Share This Article