Msanii wa Bongo Fleva Lucas Mkenda aka Mr. Nice ametangaza kuhamishia muziki wake nchini Kenya, kutokana na kile alichokitaja kuwa kufanyiwa figisu nchini mwao Tanzania katika tasnia ya muziki.
Mr. Nice ambaye alitia fora mapema mwaka 2000 kutokana na vibao kama vile Fagilia,1st Lady, na Kikulacho amepasua ukemi na kusema kuwa kikubwa kilichomfanya kuhamishia kazi yake Kenya ni kutokana na Watanzania kutofurahia wala kuithamini kazi yake ya sanaa.
Mr. Nice alikuwa maarufu sana kutokana na vibao vyake na yamkini alifikia kipindi cha kufilisika ndiposa akahiari kuhamia Kenya.