Mpiganiaji uhuru Field Marshall Muthoni Kirima afariki

Martin Mwanje
1 Min Read
Field Marshall Muthoni Kirima

Mpiganiaji uhuru wa taifa hili Field Marshall Muthoni Kirima amefariki.

Hadi kufariki kwake, alikuwa na umri wa miaka 92.

Taarifa za kufariki kwake zimetolewa na Naibu Rais Rigathi Gachagua leo Jumanne asubuhi.

“Nimeamka kwa taarifa za kuhuzunisha kwamba Field Marshall Muthoni Kirima, mpiganiaji uhuru mashuhuri aliyepigana bega kwa bega na Field Marsall Dedan Kimathi Wachiuri katika misitu ya Mlima Kenya na Aberdare kuwafurusha wakoloni kutoka nchi yetu amefariki,” alisema Gachagua wakati akitoa taarifa za kifo cha mwenda zake.

“Naungana na familia na warithi wa vita vya ukombozi vya Mau Mau katika kuomboleza kifo cha Mama yetu Field Marshall Muthoni wa Kirima.”

Naibu Rais akiongeza kuwa taifa hili daima linawashukuru mashujaa hao wa vita waliojitolea kwa udi na uvumba kupigania ukombozi wa taifa hili.

Share This Article