Mpango wa lishe shuleni wapongezwa Elgeiyo Marakwet

Tom Mathinji
1 Min Read

Wadau katika sekta ya elimu kutoka kaunti ya Elgeyo Marakwet, wamepongeza mpango wa lishe shuleni kwa shule za Kutwa wakisema mpango huo umeleta matokeo bora kwa shule tangu kuanzishwa kwa mpango huo.

Wakizungumza wakati wa kutoa chakula kwa takribani wanafunzi 7,000 kutoka shule 26 za kutwa kutoka shirika la kushughulikia maswala ya watoto(Child Welfare Society of Kenya) kwa ushirikiano na afisi ya mbunge wa eneo la Keiyo kusini, wadau hao wamesema awali wanafunzi wamekuwa wakikumbana na jinamizi la njaa hali ambayo imewalazimu wengi wao kusitisha masomo na kuanza vibarua ili kukimu maisha.

Wadau hao sasa wana imani kuwa shule hizo zitasajili matokeo bora zaidi mwaka huu kwani wanafunzi sasa wana wana muda wa kutosha wa kusoma.

Kulingana na maafisa kutoka shirika hilo mpango huo unanuia kufaidi maelfu ya wanafunzi kutoka shule za kutwa more nchini.

Share This Article