Motsepe hatimaye akubali kutetea Urais wa CAF mwakani

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa shirikisho  la kandanda barani Afrika CAF Dkt.Patrice Motsepe, ametanagza kuwania muhula mwingine wa miaka minne afisini kwenye uchaguzi ulioratibiwa kuandaliwa Machi 25 mwakani.

Motsepe aliye na umri wa miaka 62 alichaguliwa kinara wa CAF mwezi Machi mwaka 2021, alipata uungwaji mkono kutoka kwa Rais wa shirikisho la kandanda Ulimwenguni Giani Infantino.

Awali Motsepe alikuwa hajafanya uamuzi iwapo atatetea kiti chake au la hali ambayo ilikuwa imeanza kuibua maswali chungu nzima.

Motsepe ni Rais wa 7 wa shirikisho la CAF tangu libuniwe mwaka 1957.

Share This Article