Moto wazuka katika shule ya upili ya wasichana ya Isiolo

Tom Mathinji
1 Min Read
Shule ya upili ya wasichana ya Isiolo yateketea.

Moto umezuka katika bweni moja la shule ya upili ya wasichana ya Isiolo, Jumamosi usiku.

Chanzo cha moto huo hakijabainishwa, lakini shirika la msalaba mwekundu kupitia mtandao wa X, limesema limetuma maafisa wake wa dharura kusaidia katika shughuli za uokoaji.

“Moto umezuka katika shule ya upili ya wasichana ya Isiolo, kaunti ya Isiolo. Kikosi cha dharura kimetumwa katika eneo hilo,” lilisema shirika hilo kupitia mtandao wa X.

Katika kanda za video zilizoonekana na shirika la KBC, wakazi wa eneo hilo wanaonekana wakijaribu kuwaokoa wanafunzi na kujaribu kuzima moto huo.

Tukio hilo limejiri siku mbili tu baada ya moto kuteketeza bweni la shule ya Hillside Endarasha na kusababisha vifo vya wanafunzi 18.

TAGGED:
Share This Article