Nyaraka muhimu zimeteketea baada ya moto kuzuka kwenye kituo cha kuzihifadhi katika majengo ya bunge la kaunti ya Migori.
Moto huo ulizuka muda mchache baada ya wakaguzi kuondoka kwenye majengo ya bunge hilo.
Chanzo cha moto huo hakijabainika.
Polisi wameanzisha uchunguzi kubaini kilichosababisha moto huo huku baadhi wakikisia kuwa huenda kuna njama ya kuficha ukweli kuhusiana na matumizi ya fedha kwenye bunge la kaunti hiyo.