Moto wateketeza majumba Dar es salaam

Marion Bosire
0 Min Read

Moto mkubwa umeteketeza kituo cha mafuta cha Big Bon na majumba yaliyo karibu katika eneo la Kariakoo, mkoa wa Dar Es Salaam nchini Tanzania.

Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo alisema kwamba juhudi zinatekelezwa ili kudhibiti moto huo ambao chanzo chake hakijabainika.

Unasemekana kuathiri majengo kama matano likiwemo Big Bon ambalo linasheheni afisi za Benki ya Afrika – BOA.

Share This Article