Morocco yawaachilia huru wafungwa 5,000 wa bangi

Dismas Otuke
1 Min Read

Mfalme wa Morocco Mohammed wa VI ametoa msamaha na kuwaachilia huru wafungwa 5,000 waliopatikana na bangi.

Taifa hilo la Afrika Kaskazini ni mojawapo ya mataifa yanayokuza bangi kwa wingi kwa matumizi ya dawa tangu mwaka 2021, lakini haliruhusu bangi hiyo kutumiwa kwa uraibu.

Morocco ilinakili mavuno ya metric tani 294 ya bangi mwaka 2023, ambayo nyingi yake iliuzwa nje ya nchi.

Taifa hilo linatarajiwa kunakili mavuno makubwa mwaka huu, baada ya serikali kutoa leseni kwa wakulima wengi kukuza zao hilo.

Bangi hukuzwa kwa wingi maeneo ya kaskazini mwa Morocco ambayo pia inalenga soko la kimataifa ambalo lilipokea leseni 54 za kuuza bangi nje ya nchi mwaka uliopita.

Website |  + posts
Share This Article