Morocco walitwaa taji ya FIBA AfroCan katika mpira wa kikapu baada ya kuwashinda Ivory Coast alama 78-76 kwenye fainali iliyoandaliwa juzi Jumapili mjini Luanda nchini Angola.
Yalikuwa matokeo bora kwa Morocco baada ya kumaliza ya nne katika makala ya kwanza nwaka 2019 jijini Bamako nchini Mali.
Ivory Coast walishinda robo ya kwanza 25-22 kabla ya Morocco kutwaa robo ya pili 21-11 na kushinda tena seti ya tatu 14-13 na hatimaye Ivory Coast wakashinda seti ya mwisho 27-21.