Morocco yatinga nusu fainali AFCON U-23

Dismas Otuke
2 Min Read
Ismael Saibari of Morocco celebrates goal with teammates during the 2023 U23 Africa Cup of Nations match between Morocco and Ghana held at Prince Moulay Abdallah Stadium in Rabat, Morocco on 27 June 2023 ©Ladjal Djaffar/BackpagePix

Morocco walitawala mchuano wa kundi A uliosakatwa uwanjani Prince Moulay Abdellah jijini Rabat Jumanne usiku.

Atlas Lions walichukua uongozi kunako dakika ya saba kupitia kwa bao la Amir Richardson aliyeunganisha pasi murua kutoka kwa Adel, kabla ya Ismail Sabiri kutanua uongozi dakika 6 baadaye.

Ismael Saibari wa Morocco akisherehekea bao na wenzake

Yanis Begraqoui aliongeza goli la tatu dakika ya 30 huku Ghana walijipatia bao la maliwazo kupitia kwa Salim Adams, dakika mbili kabla ya mapumziko.

Adel na Begraoui waliongeza goli moja kila mmoja kwa wenyeji katika ushindi huo mkubwa.

Ushindi huo unawahakikishia Morocco kumaliza katika nafasi ya kwanza kutoka kundi A huku wakiratibiwa kuchuana na Congo katika mechi ya kuhitimisha ratiba ya kundi Jumamosi.

Morocco wanaongoza kundi hilo kwa pointi 6 baada ya kuwashinda Guinea katika mechi ya ufunguzi.

Katika pambano la awali siku ya Jumanne kundini A, Congo waliyaaga mashindano baada ya kuambulia kichapo cha magoli 3-1 dhidi ya Guinea.

Kipute hicho kitaendela Jumatano kwa mechi mbili za kundi B, mabibgwa watetezi Misri wakikabana koo na Mali uwanjani Ibn Batouta mjini Tangier, katika mechi ambayo ni sharti Pharoes washinde ili kuwa na fursa ya kuibukia nusu fainali baada ya kutoka sare tasa na Niger katika mchuano wa ufunguzi.

Baaday,e Gabon watamenyana Niger katika mechi ya kundi B.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *