Timu ya taifa ya wanaume ya mpira wa vikapu Kenya Moran’s ilifuzu kwa robo fainali ya michuano inayoendelea ya FIBA Afrocan licha ya kushindwa alama 63-66 na Gabon kwenye mechi yake ya pili ya kundi A mjini Luanda, Angola.
Kenyan Morans ilikabiliwa na ukinzani mkali kwenye robo ya kwanza walionyakua alama 16-15. Morans ilishinda robo ya pili alama 16-12 na kulazimu mechi hiyo kwenda mapumzikoni Kenya ikiongoza alama 32-27.
Aidha, Gabon ilirejea kwa vishindo na kushinda robo ya tatu na nne alama 27-18 na 13-12 mtawalia na kuandikisha ushindi wa alama 66-63.
Kikosi hicho cha kocha Cliff Owuor kilimaliza katika nafasi ya kwanza Kundini A mbele ya Kodivaa na Gabon.
Kenya Morans ilishindwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenye fainali ya makala ya mwisho mwaka 2019.