Moraa asajili rekodi mpya ya mita 800 Silesia

Dismas Otuke
2 Min Read

Bingwa wa jumuiya ya madola Mary Moraa,aliendeleza msururu wa matokeo bora mwezi mmoja kabla ya mashindanoi ya riadha duniani, alipoibuka mshindi wa mita 800 katika mashindanio ya Diamond league yaliyoandaliwa mjini Silesia Poland Jumapili usiku.

Moraa aliziparakasa mbio hizo huku akiweka rekodi mpya ya mashindano hayo na pia muda bora wa msimu wa dakika 1 sekunde 56 nukta 85.

Moraa ndiye Mkenya pekee aliyeibuka mshindi katika mkondo huo wa nane wa Diamond League.

Halimah Nakaayi wa Uganda alimaliza wa pili kwa dakika 1 sekunde 57 nukta 78 ikiwa rekodi mpya ya kitaifa wakati Natoya Goule, kutoka Jamaica akiridhia nafasi ya tatu kwa dakika 1 sekunde 57 nukta 90,ukiwa muda wake bora wa msimu.

Lillian Kassait alimaliza wa pili katika mita 3,000 akitumia dakika 8 sekunde 27 nukta 80,nyuma ya Freweyni wa Ethiopia ,aliyetwaa ushindi kwa mud awa rekodi mpya ya mashindano ya dakika 8 sekunde 26 nuktab 61.

Teressia Muthoni ambaye ni bingwa wa dunia kwa chipukizi mwaka 2020,alichukuwa nafasi ya nne.

Katika matokeo ya wanaume Abel Kipsang, alisajili muda bora wa kibinafsi alipokamilisha wa pili katika mita 1500 akitumia dakika 3 sekunde 29 nukta 11,nyuma ya Jakob Ingebrigsten wa Norway aliyeweka rekodi mpya ya mashindano ya dakika 3 sekunde 27 nukta 14.

Reynold Kipkorir alimaliza katika nafasi ya tatu kwa mud awa dakika 3 sekunde 30 nukta 30.

Abraham Kibiwot na Leonard Bett walimaliza katika nafasi za pili na tatu mtawalia katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji nyuma ya mshindi Soufiane El Bakkali wa Morocco, aliyesajili rekodi mpya ya mashindano ya dakika 8 sekunde 3 nukta 16.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *