Mnyama Simba ashinda mechi ya kwanza Uarabuni

Dismas Otuke
1 Min Read

Miamba wa soka Tanzania bara klabu ya Simba waliliwashinda SC Sfaxien  ya Tunisia bao moja kwa bila katika mechi ya kundi A, kuwania kombe la Shirikisho iliyosakatwa jana  nchini Tunisia.

Ushindi huo ulikuwa wa pili mtawalia kwa Simba dhidi ya Waarabu hao na pia ukiwa ushindi wa kwanza kwa Simba katika mechi za kimataifa dhidi ya timu ya Uarabuni.

Jean Ahoua alipachika bao pekee na la ushindi kwa timu ya wenye nchi kunako kipindi cha kwanza, baada ya kufyatua fataki kutoka nje ya kijisanduku.

Kufuatia ushindi huo Simba wanaongoza kundi hilo kwa pamoja na  CS Constantine ya Algeria kwa alama 9  baada ya mechi nne huku FC Bravos Do Maquis ya Angola ikiwa ya tatu kwa alama 6 wakati Sfaxien wakishika nanga pasi na alama.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *