Mnangagwa ashinda muhula wa pili wa Urasi Zimbabwe

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa zimbabwe Emmerson Mnangagwa, ameshinda muhula wa pili kwenye uchaguzi mkuu ulioandaliwa Agosti 23 akigombea kwa tiketi ya chama cha ZANU-PF huku upinzani ukipinga matokeo hayo ambayo pia yametiliwa shaka na waangalizi.

Mnangagwa,amepata asilimia 52 nukta 6 ya kura zote huku mpinzani wake wa karibu Nelson Chamisa akipata asilimia 44 kwenye matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi nchini Zimbabwe ZEC Jumamosi usiku.

Mnangagwa alitwaa mamlaka mwaka 2017 kufutia mapinduzi ya kijeshi yaliyomng’atua marehemu Robert Mugabe.

Uchaguzi huo mkuu uligubikwa na ucheleweshwaji wa kutangazwa kwa matokeo hali iliyochangia upinzani kuhisi kuwa ulikumbwa na wizi wa kura kauli iliyoungwa mkono na waangalizi wa kimataifa waliosema Ijumaa kuwa uchaguzi huo haukuafiki viwango vilivyohitajika.

Kulingana na tume ya ZEC ,Mnangagwa aliye na umri wa miaka 80 alizoa jumla ya kura milioni 2 nukta 3 dhidi ya Chamisa aliyepata kura milioni 1 nukta 9.

Share This Article