Mwanamke mwenye umri wa miaka 55, amehukumiwa kifungo cha miaka 50 jela, baada ya kupatikana na hatia ya ulanguzi wa mihadarati aina ya heroin.
Ikitoa hukumu hiyo Jumanne, Mahakama moja ya Busia ilimhukumu kifungo hicho Mwaura Mumbi au alipe faini ya shilingi milioni 50, baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha kesi dhidi yake.
Mumbi, alipatikana na hatia ya ulanguzi wa dawa za kulevya kinyume na sehemu ya 4(a)(ii) ya sheria za kukabiliana na mihadarati nambari ya mwaka 2022.
Mshukiwa huyo alitiwa nguvuni Machi 10, 2023 katika kituo cha mpakani cha Busia akiwa na kilo 3.9 za heroin zinazokisiwa kuwa za shilingi milioni 11.8.
Upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi mahakamani, huku mahakama ikikubaliana na ushahizi uliotolewa mbele yake.