Kamanda wa jeshi la nchi kavu Luteni Jenerali Peter Njiru, anashiriki mkutano wa amani na wakuu wengine wa jeshi katika eneo la bahari Hindi na Pasifiki nchini India.
Mkutano huo unalenga kuimarisha ushirikiano wa kijeshi katika kuleta amani na uthabiti katika eneo hilo.
Aidha utatoa fursa ya ushirikiano kati ya majeshi ya nchi kavu katika kanda hiyo ili kuwa na maono sawa na kuwezesha kanda hiyo kushughulikia fursa zilizopo katika karne hii ya 21.
Wakuu hao wa jeshi la nchi kavu, pia wataangazia ubadilishanaji wa mbinu bora za kukabiliana na dharura za kimazingira katika kanda hiyo.
Wakuu wa jeshi kutoka zaidi ya mataifa 30 wanahudhuria mkutano huo.