Mkurugenzi wa zamani wa KEMRI Davy Koech afariki

Dismas Otuke
1 Min Read

Mkurugenzi wa zamani wa taasisi ya matibabu nchini (KEMRI) Dkt Davy Koech, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 73, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Koech alipatikana na hatia na mahakama ya kupambana na ufisadi nchini kwa kuhamisha shilingi milioni 19.3, zilizotengewa kituo cha kudhibiti magonjwa kwa kaunti ya Kisumu hadi katika akaunti ya kibinafsi.

Alihukumiwa kifungo cha miaka sita gerezani kwa kosa hilo lakini akasemehewa na Rais William Ruto mwaka 2023.

Share This Article