Mkurugenzi wa CA Ezra Chiloba asisitiza usalama wa watoto mitandaoni

Martin Mwanje
2 Min Read

Matumizi ya intaneti yanaweza yakawafanya watoto kukumbwa na hatari wasipohamasishwa kwa kupewa habari ili kujilinda wenyewe.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini, CA Ezra Chiloba anasema ingawa intaneti ni lango kuelekea fursa zisizokuwa na ukomo, usalama wa watoto mitandaoni ni muhimu kuhakikisha watoto wananufaika kutokana na matumizi ya intaneti.

“Watumiaji ni washikadau muhimu, hasa watoto na vijana, kwani wao huanza kutumia mapema bidhaa na huduma za Habari, Mawasiliano na Teknolojia, ICT. Ili kuhamasisha matumizi yenye tija ya intaneti na kubuni tajiriba salama ya intaneti, kuna haja ya washikadau mbalimbali kuendelea kushirikiana,” alisema Chiloba wakati wa Tamasha Inayoendelea ya Filamu Nchini mjini Nyeri.

CA ni mfadhili mkuu wa “Uhifadhi na Usalama wa Watoto Mitandaoni” kwa mwaka wa tano mfululizo ikiangazia hasa “Uhamasishaji wa Matumizi Salama ya Intaneti, Tabia Nzuri Mitandaoni, Uepukanaji wa Tabia Potovu Mitandaoni, na Kuhifadhi Kutambuliwa na Sifa Yako Mitandaoni.”

“Kuendelea kwetu kuunga mkono Tamasha ya Kitaifa ya Muziki Nchini ni njia moja ya CA kukuza uelewa kuhusu suala hili muhimu. Tamasha hii ilituwezesha kufikia lengo hili wakati tukiwatia moyo watoto na vijana kunadi vipaji vyao kupitia muziki na densi,” aliongeza Chiloba.

Miaka iliyopita, tamasha hiyo imeibuka kuwa njia bora ya kukuza maadili bora miongoni mwa watoto na vijana nchini.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *