Mkurugenzi Mkuu wa KAA atozwa faini ya shilingi 500,000

Tom Mathinji
2 Min Read

Bunge la taifa limemtoza faini ya shilingi 500,000 Mkurugenzi Mkuu wa halmashauri ya kusimamia viwanja vya ndege nchini KAA Henry Ogoye, kwa kukosa kufika mbele ya bunge hilo.

Mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu maridhiano na fursa sawa Adan Haji, alisema Mkurugenzi huyo alitozwa faini hiyo baada ya kukosa kufika mbele ya kamati hiyo mara nne, kuelezea kuhusu uajiri wa wafanyakazi na maswala mengine.

“Kamati hiyo imechukua hatua kuambatana na ehemu ya  191 A (1) ambayo inaipa kamati hiyo mamlaka ya kumtoza faini yeyote anayekosa kufika mbele yake,” alisema mbunge huyo wa Mandera Magharibi.

Wakati wa mkutano huo ulioongozwa na Haji katika majengo ya Leo Alhamisi, wanachama wa kamati hiyo walielezwa ghadhabu yao baada ya Mkurugenzi huyo kukaidi maagizo ya kufika mbele yao.

“Hii ni mara ya nne Mkurugenzi huyo amekosa kufika mbele ya kamati mara nne…hii ndio sababu tumechukua hatua dhidi yake,” alisema Haji.

Kwa upande wake mbunge wa Kajiado Kaskazini Onesmus Ngogoyo, alisema kamati hiyo haitawasaza maafisa wakuu wa serikali wanaokosa kuheshimu maagizo ya kamati kufika mbele yake.

“Mashahidi wanapaswa kutulia maanani mwaliko wa kufika mbele ya kamati za bunge,’ alisema Ngogoyo.

Ogoye alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo kuelezea kuhusu mikakati iliyowekwa kuhakikisha wakenya wote wanapata fursa sawa za kiajiriwa katika halmashauri hiyo.

Share This Article