Mkondo wa tatu wa mbio kuandaliwa Eldoret wikendi hii

Dismas Otuke
1 Min Read

Mkondo wa tatu wa mbio na mashindano ya viwanjani utaandaliwa  kati ya tarehe 14 na 15 mwezi huu, katika uwanja wa Eliud Kipchoge Sports Complex  kaunti ya Uasin Gishu.

Mkondo huo utashirikisha  fainali za mita 100,400,400 kuruka viunzi,800,1500,3,000 kuruka viunzi na maji,5,000 na 10,000 kwa wanaume na wanawake.

Mashindano ya viwanjani ni pamoja na shot Put,Javelin na Long Jump kwa wanaume na wanawake.

Mkondo huo unafuatia mikondo ya Kakamega na Thika iliyoandaliwa mwezi jana.

 

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *