Mkondo wa kwanza wa mbio za nyika kuandaliwa kesho Iten

Dismas Otuke
1 Min Read

Mkondo wa kwanza wa mbio za nyika utaandaliwa kesho mjini Iten,yakiwa mashindano ya kufungua kalenda ya chama cha Riadha Kenya msimu wa mwaka 2024/2025.

Mkondo huo wa kwanza utafuatwa na wa Kapsokwony  Oktoba 26 na Machakos tarehe 2 Novemba kwa mkondo wa tatu.

Kaunti ya Bomet Itaandaa mkondo wa nne Novemba 30 na ule wa tano Disemba 14 na hatimaye ule wa Kisii Januari 6 mwaka ujao.

Kulingana na Mkurugenzi wa riadha ya vijana katika chama cha Riadha Kenya ,Barnaba Korir wamejiandaa vyema kwa msimu mpya na uteuzi wa timu Dhabiti  kwa mashindano ya riadha Duniani mwaka ujao mjini Tiokyo Japan.

“Tuko tayari kwa simu tunaanzia Iten lakini pia mashindano makubwa ambayo tunayaandaa ni Chepsaita Cross Country ambayo yameidhinishwa na shirikisho la Riadha duniani yakiwa ya kwango cha dhahabu Disemba mwaka huu,mbio za Sirikwa Classic mwezi Februari na pia Kip Keino Classic mwezi Mei mwaka ujao.”

TAGGED:
Share This Article