Mkewe rais Rachel Ruto aanzisha mpango wa mashamba ya matunda shuleni

Marion Bosire
1 Min Read

Afisi ya mke wa rais Bi. Rachel Ruto kupitia kwa shirika lake la “Mama Doing Good” imeanzisha mpango wa mashamba ya matunda shuleni, kote nchini.

lengo la mpango huo ni kuhakikisha lishe bora kwa wanafunzi na kusaidia shule kujipatia mapato.

Shule ya kwanza kabisa ambayo imefaidi na mpango huo ni shule ya msingi ya Kimondi ambayo iko katika kaunti ya Nandi.

Wanafunzi wa shule hiyo ya msingi, walipokea miche ya parachichi kutoka kwa afisi ya mkewe rais ambayo walipanda kwenye ardhi ya shule yao.

Wawakilishi wa shirika la Mama Doing Good, pia waliwapa wanafunzi wa kike sodo ili kuhakikisha hakuna yeyotekati yao anakosa kufika shuleni kwa sababu ya hedhi.

Naibu gavana wa kaunti ya Nandi Daktari Yulita Chebotip Cheruiyot alishukuru afisi ya mke wa rais kwa hatua ya kuanzisha mashamba ya matunda shuleni na kwa kusaidia watoto wa kike kusalia shuleni hata wanapopitia jambo la kawaida kimaumbile.

Shirika la Mama Doing Good hujihusisha na mipango mbali mbali kwa ushirikiano na wadau mbali mbali ambayo inasaidia katika kuinua jamiikwa jumla.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *