Mke wa mwigizaji na mchekeshaji Makokha ambaye jina lake halisi ni Matayo Keya, kwa jina Purity Wambui amefariki. Wambui anasemekana kufariki mwishoni mwa juma lililopita akipokea matibabu.
Mwigizaji mwenza wa Makokha, Hiram Mungai almaarufu Ondiek Nyuka Kwota ndiye alitangaza kifo cha Wambui kupitia mitandao ya kijamii ambapo alimsifia kama mama ambaye aligusa wengi na moyo wake wa kusaidia.
“Matayo Keya, ambaye pia anafahamika kama Makokha Makacha na familia yake wameshukuru sana kwa upendo wenu na usaidizi wakati huu mgumu.” aliandika Ondiek.
Ondiek aliwataka wafuasi wa Makokha kwenye mitandao ya kijamii kuendelea kuiombea na kuisaidia familia yake.
Wambui hakuwa anajulikana sana kama mume wake.
Tunamtakia Makokha na familia yake faraja wakati huu wa majonzi.