Refarii wa Kenya Peter Waweru Kamaku ameteuliwa kuwa mwamuzi mkuu wa mechi ya kundi F ya kombe la AFCON kati ya Morocco na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo .
Kamaku aliye na umri wa miaka 39 ni Profesa wa Hisabati katika chuo kikuu cha JKUAT, na atakuwa akiwa mwamuzi mkuu katika fainali za mwaka huu nchini Ivory Coast kwa mara ya kwanza.
Refa huyo alikuwa akisamamia mtambo wa VAR alipoipa Misri penati iliyowapa sare ya 2-2 dhidi ya Msumbiji katika pambano la ufunguzi la kundi B.
Gilbert Cheruiyot na Stephen Yiembe, ndio waamuzi wasaidizi wa Kenya kwenye kipute cha mwaka huu nchini Ivory Coast.