Mkahawa wa kifahari wa The Hilton utafunga tawi lake la katikati ya jiji la Nairobi Disemba 31 mwaka huu, baada ya kuhudumu kwa zaidi ya miongo mitano.
Wafanyikazi wote wanaohudumu katika Hoteli hiyo watapoteza kazi zao.
Mkahawa wa Hilton unamilikiwa na serikali kwa asilimia 40 nukta 70 .
Wasimamizi wa Hoteli ya Hilton wamesema hawatafunga biashara nchini Kenya bali tawi hilo tu la katikati ya jiji huku wakiendelea kuhudumu katika matawi yake mengine nchini.
Hoteli ya Hilton tawi la Nairobi ilianza shughuli zkae Disemba 17 mwaka 1969 na ilifunguliwa rasmi na Rais wa kwanza wa Kenya Mzee Jomo Kenyatta.
Tawi la Hilton katikati ya jiji linajumuisha vyumba vya kulala 287,vyumba 185 vyenye vitanda viwili,vyumba vyenye chemba mbili 45, vyumba 27 vya kifahari miongoni mwa huduma nyingine za kibwenyenye.