Mitihani ya kitaifa ya darasa la nane KCPE na tathmini ya gredi ya sita ya KPSEA ya mwaka huu, imekamilika rasmi.
Mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE wa mwaka huu ndio wa mwisho katika mtaala wa 8-4-4, ambao umedumu miaka 38.
Kulingana na katibu katika wizara ya elimu Dkt. Belio Kipsang’g alisema wanafunzi milioni 1.4, walisajiliwa katika mtihani wa mwaka huu wa KCPE, akidokeza kuwa hii ndio idadi ya juu zaidi ya wanafunzi kufanya mtihani huo katika historia ya nchi hii.
Wanafunzi wa darasa la nane KCPE walifanya mtihani wa mwisho wa somo la jamii na dini Jumatano asubuhi.
Viongozi kadhaa wakiongozwa na Rais William Ruto, walizuru vituo mbalimbali vya mitihani kufungua na kusambaza karatasi za mitihani.