Mitihani ya KCPE na KPSEA kuanza leo Jumatatu kote nchini

Tom Mathinji
1 Min Read
Mtihani wa KCPE na KPSEA wakamilika.

Watahiniwa wa darasa la nane na wanafunzi wa gredi ya sita, wanaanza mitihani yao ya kitaifa hivi leo Jumatatu.

Watahiniwa wa darasa la nane watafanya mtihani wa kitaifa wa KCPE huku wale wa gredi ya sita wakifanya tathmini ya KPSEA.

Mitihani hiyo itaanza leo Jumatatu na kukamilika Jumatano tarehe mosi mwezi Novemba.

Watahiniwa 1,282,574 watafanya tathmini ya KPSEA. Watahiniwa watakaofanya mtihani wa KCPE mwaka huu ni 1,415, 315.

Watahiniwa 170,982 zaidi walisajiliwa kwa mtihani wa KCPE mwaka huu ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Kinyume na mitihani ya KCPE ambapo alama  jumla ni asilimia 100, mtihani wa KPSEA utakuwa na alama 40 pekee.  Alama 60 zilizosalia zitatokana na mitihani ya utathmini itakayofanywa darasani katika gredi za 4, 5 na 6.

Mtihani wa mwaka huu wa KCPE unafanywa kwa mara ya mwisho,na kuashiria mwisho wa mfumo wa elimu wa 8-4-4 .

TAGGED:
Share This Article