Misri kuandaa kipute cha AFCON kwa chipukizi chini ya miaka 20

Dismas Otuke
1 Min Read

Misri imepokezwa maandalizi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 20, kuanzia tarehe 27 mwezi ujao na shirikisho la CAF.

Hii inafuatia kujiondoa kwa waandalizi wa awali Ivory Coast, kutokana na kile serikali ilitaja kuwa sababu zisizoepukika.

Misri ilikuwa imetuma maombi ya kuwa mwenyekiti wa fainali hizo kabla ya kushindwa na Ivory Coast.

Makala ya mwaka huu yataandaliwa kati ya April 27 na Mei 18.

Kenya imejumuishwa kundi C pamoja na Zambia, Sierra Leone na mabingwa watetezi Senegal.

Junior Stars wa Kenya ambao wako kambini watafungua ratiba dhidi ya Sierra Leone Mei mosi, kabla ya kumenyana na Zambia Mei 4, na kufunga ratiba dhidi ya Senegal Mei 7.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *