Miradi ya maji yabadili taswira Kwale

Marion Bosire
1 Min Read

Wakazi katika maeneo kame ya Lunga Lunga na Kinango kwa muda mrefu wamekuwa wakitegemea chakula cha msaada kutokana na maeneo hayo kukumbwa na kiangazi mara kwa mara.

Ni hali iliyosababisha wakazi laki moja kutegemea chakula cha msaada kila mwaka.

Hata hivyo, taswira katika maeneo husika inaendelea kubadilika kutokana na ujenzi wa mabwawa 17 katika maeneo ya Kinango na LungaLunga yanayoendeleza kilimo cha unyunyiziaji maji mashamba.

Kufikia sasa, zaidi ya ekari 200 za mashamba ziko chini ya kilimo cha unyunyizaji maji mashamba.

Mabwawa ya Nyalani Kizingo na Mwaluvuno katika eneo la Kinango, na Mwakalanga katika eneo la Lunga Lunga ni miongoni mwa miradi ya mabwawa iliyoleta mageuzi katika sekta ya kilimo katika kaunti ya Kwale.

Miradi hiyo imewawezesha wakulima kuendeleza shughuli zao hata nyakati za kiangazi.

Share This Article