Taarifa ya Kimutai Murisha
Kaunti ya Nandi inakabiliwa na idadi kubwa ya mimba za mapema na visa vya ubakaji, hasa katika eneo bunge la Tindiret, ambapo takriban asilimia 23 ya wale wanaozaa ni wasichana wenye umri mdogo.
Hali hiyo inaathiri elimu , afya na maisha yao kwa jumla.
Kulingana na Mkurugenzi wa Masuala ya Jinsia katika kaunti ya Nandi, George Odunga, mwaka jana, wasichana 991 katika eneo bunge la Tindiret walipata ujauzito wakiwa wamebaleghe.
Ni hali ambayo imemfanya Kamishna wa kaunti hiyo Wilberforce Kilonzo kuonya vijana katika taasisi za elimu kukoma kuwachumbia wasichana wadogo akionya kuwa watakaopatikana watachukuliwa hatua kali za kisheria.