Mike Sonko azoa tuzo ya mhisani bora Afrika Mashariki

Alitunukiwa tuzo hiyo kwenye tuzo za E360 Ijumaa jijini Nairobi

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanasiasa Mike Sonko alijizolea tuzo ya mhisani bora katika eneo la Afrika Mashariki katika tuzo za E360 Entertainment zilizoandaliwa Ijumaa jioni katika ukumbi wa Nairobi Cinema.

Sonko ambaye pia alikuwa amealikwa kama mgeni rasmi wa tuzo hizo alishukuru kwa kutambuliwa na waandalizi wa tuzo hizo.

Alisema tuzo hiyo ni udhihirisho wa kazi za kibinadamu ambazo amekuwa akifanya za kusaidia waliotelekezwa katika jamii.

“Ninatoa tuzo hii kwa wote walionufaika kutokana na mipango yetu mbali mbali chini ya mwavuli wa Sonko Rescue Team.” Aliandika Sonko kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Kiongozi huyo hakuweza kuhudhuria hafla hiyo na anamshukuru Nicko Nyamai afisa wake wa mahusiano na vyombo vya habari aliyepokea tuzo hiyo kwa niaba yake.

Sonko anafahamika sana kwa kusaidia watu mbali mbali katika jamii kupitia kwa shirika alilobuni la kusaidia jamii almaarufu Sonko Rescue Team.

Hivi maajuzi amemchukua mtoto ambaye alibaki yatima baada ya kushuhudia babake akiuawa na wezi kwa kuchomwa kisu mara kadhaa na sasa yeye ndiye babake mlezi.

Picha zake na za mtoto huyo wa kiume zilionyeshwa wakati wa kutoa tuzo hiyo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *