Miili minne imepatikana imetuowa kwenye shamba moja la mahindi mapema Jumapili karibu na kambi ya jeshi ya Moi mjini Eldoret.
Walioshuhudia kisa hicho walisema miili hiyo ilikuwa imetupa kndani ya mtaro ikiwa na majeraha ya risasi.
Kulingana na Kamanda wa polisi wa kaunti ya Uasin Gishu Benjamin Mwanthi,uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha mauaji hayo.