Miili mingine 12 yafukuliwa Shakahola

Martin Mwanje
1 Min Read

Miili 12 zaidi imefukuliwa katika msitu wa Shakahola leo Jumatatu.

Kufukuliwa kwa miili hiyo kunafikisha 403 jumla ya miili ambayo imefukuliwa katika msitu wa Shakahola tangu kuanza kwa shughuli ya upekuaji na ufukuaji wa makaburi katika msitu huo.

Waliofariki wanashukiwa kuwa wafuasi wa dhehebu la Good News International linaloongozwa na mhubiri tata Paul Mackenzie.

Idadi ya manusura inasalia 95 huku watu 37 wakiwa wamekamatwa kuhusiana na kisa hicho.

Kwa mujibu wa Kamishna wa kanda ya Pwani Rhoda Onyancha, miili 258 imefanyiwa uchunguzi wa vinasaba, yaani DNA hadi kufikia sasa.

Shughuli ya ufukuaji wa makaburi itaendelea kesho Jumanne.

Taarifa ya Dickson Wekesa

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *