Mibabe wa riadha kuvaana Jumamosi Kip Keino Classic

Dismas Otuke
2 Min Read

Wanariadha mashuhuri kutoka pembembe mbli mbali za dunia wamo nchini kushiriki makala ya tano ya mashindano ya Kip Keino Classic Continental Tour Jumamosi hii katika uwanja wa taifa wa Nyayo.

Baadhi ya wanariadha tajika watakaoshiriki mashindano ya Jumamosi ni mshindi wa nishani ya fedha ya dunia katika mita 100,Letsile Tebogo wa Botswana atakayetimka mita 200.

Pia washindi wa nishani za olimpiki katika mita 100 na 200 Keneth Bednarek wa Marekani na Christine Mboma kutoka Namibia  pia watashiriki.

Washiriki wa Kenya ni pamoja na bingwa wa dunia wa mita 800 Mary Moraa,mshindi wa nishani ya fedha ya dunia katika mita 800 Emmanuel Wanyonyi, huku Ferdinand Omanyala akilenga kuhifadhi taji yake ya mita 100 dhidi yaBednarek wa Marekani aliyemaliza wa pili mwaka jana.

Mashindano ya uwanjani yatawashirikisha bingwa wa dunia Ethan Katzberg wa Canada , bingwa wa Olimpiki Wojciech Nowicki kutoka Poland,bingwa mara tano wa dunia Pawel Fajdek pia wa Poland na mshikilizi wa rekodi ya dunia Anita Wlodarczyk pia wa Poland pamoja na bingwa wa Olimpiki katuka urushaji sagai mwaka 2016 Thomas Rohler wa Ujerumani.

Mashindano ya Kenya yatakuwa ya pili katika msururu wa makala 11 ya continental tour ya kiwango cha dhahabu na yatashuhudia bingwa mtetezi wa mita 100 Ferdinad Omanyala akizindua uhasama dhidi ya Keneth Bednarek wa Marekani.

Share This Article