Mgonjwa wa pili wa Ebola afariki Kenya

Dismas Otuke
1 Min Read
Dr. Patrick Amoth - Mkurugenzi Mkuu wa Afya nchini Kenya.

Wizara ya Afya ilithibistha kifo cha pili cha mgonjwa wa Ebola Ijumaa jioni akipokea matibabu katika kituo cha kujitenga.

Katibu wa huduma za matibabu Dkt.Patrick Amoth, alisema kuwa mwanamke aliye na umri wa miaka 65, aliyekuwa jamaa wa karibu wa mgonjwa wa kwanza aliyefariki pia.

Inaaminika mgonjwa huyo aliyekuwa jamaa wa karibu wa mwanaume wa kwanza aliyeaga dunia ,alianza kuwa na dalili za Ebola Oktoba 13 ,katika kituo cha kujitenga akipokea matibabu.

Serikali kupitia kwa wizara ya afya imesema itasaidia familia kumzika marehemu ili kulinda watu wengine wa familia hiyo na umma kwa jumla.

Kenya imenakili visa tisa vya Ebola pamoja na vifo viwili kufikia sasa huku wagonjwa  saba wakiendelea kupata matibabu katika vituo mbalimbali vya kujitenga.

Share This Article