Mfumo wa ufadhili elimu ya vyuo vikuu kurekebishwa

Dismas Otuke
1 Min Read
Waziri wa elimu Julius Ogamba.

Mfumo wa sasa ufadhili wa elimu ya vyuo vikuu utafanyiwa marekebisho, kabla ya kuanza kutekelezwa kikamilifu.

Waziri wa Elimu Julius Ogamba, amekiri kuwepo kwa malalamishi mengi kutoka kwa wanafunzi kuhusu kujumuishwa katika makundi ya ufadhili wasiyostahiki.

Mahakama kuu ilisitisha utekelezwaji wa mfumo huo kabla ya mahakama ya rufaa kuiruhusu serikali kuendelea na utekelezaji wake.

Akizungumza jana katika kaunti ya Homa Bay, waziri alisema serikali itafuata agizo la mahakama ya rufaa ya kuchapisha mpangilio wa mfumo mpya, utakaowajumuisha wanafunzi wa sasa na wale wajao katika muda wa wiki mbili .

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *