Mfahamu mbabe wa kivita wa Angola Jonas Savimbi

Marion Bosire
4 Min Read

Jonas Malheiro Savimbi alizaliwa tarehe 3 Agosti mwaka wa 1934 kijijini Muhango katika mkoa wa Bié ulioko kati mwa taifa hilo la Angola. Babake LOTE alifanya kazi katika kampuni ya reli na pia alikuwa muhubiri wa kanisa la Evangelical Congregational la Angola lenye misingi ya wamishonari wa Marekani.

Alisomea shule za kikistro na baadaye akiwa na miaka 24 akapata udhamini wa masomo nchini Ureno. Akiwa huko, alijiunga na makundi ya wanafunzi kutoka mataifa yaliyo chini ya ukoloni wa ureno na ambayo yanapinga ukoloni huo. Badhi ya wanafunzi hao ni aliyekuwa rais wa kwanza wa Angola Agostino Neto wa chama cha MPLA wakati huo akisomea udaktari.

Kufuatia kuongezeka kwa vuguvugu la makundi ya wanafunzi kwa usaidizi wa vyama vya kisiasa kama kile cha kikomonisti kutaka ureno kuondoa ukoloni nchini mwao, serikali ilianzisha msako mkali wa kuwatia mbaroni. Savimbi alihofia kukamatwa hivyo akatorokea nchini Uswizi kwa msaada wa chama cha kikomonisti cha Ureno na Ufaransa na wasamaria wema wengine. Nchini humo, alipata udhamini wa kusomea masomo ya kijamii kutoka kwa wamishonaria wa marekani. Baadaye alijiunga na chuo kikuu cha Fribourg.

Mwaka wa 1960 akiwa bado Uswizi, alikutana na Holden Roberto-mwanzilishi wa chama cha kupigania uhuru wa Angola UPA ( União das Populaçoes de Angola) ambaye kwa wakati huo alikuwa anatambulika na umoja wa mataifa kwa juhudi zake za uhuru wa Angola. Mazungumzo ya kumsajili Savimbi katika chama chake kwa nia ya kuongeza nguvu kikosi hicho yalibaki kwa njia panda.

Mwishoni mwa miaka ya sitini, Savimbi aliombwa kutoa hotuba mjini Kampala nchini Uganda kwa niaba ya wanafunzi wafuasi wa chama cha MPLA. Kwenye mkutano huo, alikutana na shujaa wa KenyaTom Mboya aliyemwalika nchini humo kukutana na rais Jomo Kenyatta ambapo aliombwa kujiunga na UPA. Baada ya mkutano huo, aliwambia wanahabari wa Ufaransa Kenyatta alimshauri kujiunga na MPLA na kwa haraka akamwandikia barua Roberto kuwa amejiunga na chama chake. Barua hiyo ilipelekwa Marekani na Tom Mboya. Aliporejea Uswizi, alipigiwa simu na Roberto na kumtaka wakutane nchini mjini Kinshasa (DRC).
Savimbi aliishi nchini DRC hadi machi 1961 aliporejea Uswizi kufanya mtihani wa udaktari. Disemba 1961 alijiunga na chuo kikuu cha Lausanne kusomea sheria na siasa za kimataifa.

Septemba ya mwaka wa 1961, waafrika kutoka koloni za Ureno wanaosomea mataifa ya nje walibuni muungano wa UGEAN mjni Rabat nchini Morocco uliokuwa na uhusiano na MPLA.

Namo Disemba mwaka wa 1961, Roberto na UPA wali’anda’a mkutano kule Camp Green Lane near Philadelphia, Pennsylvania nchini Marekani kwa ushirikiano na miungano ya wanafunzi wenye uhusiano na UPA. Savimbi alihudhuria mkutano na akawa miongoni mwa wale waliounda UNEA (União Nacional dos Estudantes Angolanos). Mwaka wa 1962 kule Lucerne Uswizi, Savimbi alichaguliwa katibu mku wa UNEA.

Baada ya uhusiano wa Savimbi na UPA kunoga, alisafiri sehemu nyingi za dunia kwa niaba ya chama hicho ikiwemo ile ya umoja wa mataifa mjini New York Marekani. Kufuati juhudi hizo, alipandishwa ng’azi hadi akawa mwanachama wa wa kamati kuu ya UPA, pia ni yeye aliyeshauri PDA (Partido Democrático de Angola) kujiunga na UPA zilizozaa FINLA (Frente Nacional de Libertação de Angola) na wakati vyama vilipounda GRAE (Govêrno Revolucionário de Angola no Exílio) aprili 3 mwaka wa 1962, alichaguliwa waziri wa maswala ya kigeni.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *