Messi azinduliwa rasmi Inter Miami

Dismas Otuke
1 Min Read

Mshambulizi wa  Argentina Lionell Messi, alijulishwa rasmi kwa mashabiki wa klabu yake mpya ya Inter Miami inayoshiriki ligi kuu ya Marekani MLS.

Messi alipokelewa rasmi na mmiliki wa timu hiyo mchezaji mstaafu David Beckham na kulakiwa na mashabiki zaidi ya 20,000 walionunua tiketi zote zilizokuwa zikiuzwa ili kumtazama  sogora huyo.

Mwanandinga huyo aliye na umri wa miaka 36 anajiunga na beki Sergio Bosquets waliyecheza pamoja Barcelona.

Akiwa Barca,Messi alipiga jumla ya mabao  672 akiwa mfungaji bora wa timu hiyo aliponyakua mataji 10 ya ligi kuu,Laliga,mataji manne ya ligi ya mabingwa ulaya na vikombe 10 vya Uhispania.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *