Meli ya Urusi yashambuliwa kwa droni Libya

Vyanzo vya ndani viliambia wanahabari Jumapili kwamba raia kadhaa wa Libya na Urusi waliuawa katika shambulizi hilo lililotokea alfajiri.

Marion Bosire
1 Min Read

Meli ya Urusi imeshambuliwa kwa droni za baharini mashariki mwa Libya na kusababisha mlipuko na moto kwa mujibu wa serikali ya eneo hilo.

Vyanzo vya ndani viliambia wanahabari Jumapili kwamba raia kadhaa wa Libya na Urusi waliuawa katika shambulizi hilo lililotokea alfajiri.

Meli hiyo ilikuwa imetia nanga katika bandari ya Benghazi, karibu na kituo cha jeshi la wanamaji.

Vyanzo hivyo vilidai kuwa meli hiyo ilikuwa imebeba silaha, risasi na ndege zisizo na rubani.

Wakazi wa eneo hilo walisema walishuhudia ndege tatu zisizo na rubani zikishambulia meli hiyo.

Kampuni ya uchambuzi wa picha za setilaiti ya Vantor ilisema picha zake zilionyesha kuwa meli iliyoshambuliwa ilikuwa Merkury, ambayo ni meli ndogo ya kivita ya Jeshi la Wanamaji la Urusi.

Picha zilizopigwa Jumapili zilionyesha sehemu kubwa ya meli hiyo ikiwa imepinduka na kuzama, huku sehemu ya mbele pekee ikiwa bado inaonekana juu ya maji.

Moshi pia ulionekana ukifuka kutoka kwenye sehemu ya juu ya meli, huku mabaki ya vitu yakitapakaa kwenye gati.

Utawala wa Benghazi ulisema awali kuwa meli hiyo ilikuwa imetia nanga kwa ajili ya kujaza mafuta na kupokea mahitaji mengine chini ya makubaliano ya ushirikiano kati ya Urusi na serikali ya mashariki mwa Libya.

Share This Article