Meli ya kifahari ya watalii yatia nanga Mombasa

Tom Mathinji
1 Min Read

Bandarinya ya  Mombasa Jumamosi asubuhi ilikuwa mwenyeji wa meli ya kifahari ya watalii ambayo inamilikiwa na kampuni ya safari za meli ya Mediterranean.

Meli hiyo imewabeba watalii 2,500 kutoka mataifa tofauti pamoja na wafanyakazi 1,000 ambapo 20 kati yao ni raia wa Kenya.

Ikiwa na urwfu wa mita 294, meli hiyo MSC Poesia, ni mojawepo wa meli kubwa zaidi kutia nanga katika bandari hiyo, mwezi mmoja baada ya meli nyingine ya kifahari ya Norway kustia nanga.

Halmashauri ya bandari nchini KPA katika mtandao wake wa  X, ilisema imewekeza katika miundomsingi ili kupiga jeki utalii wa safari za majini.

Hii inajumuiaha kituo cha kisasa cha kutia nanga kwa meli, ili kutoa fursa ya kutia nanga sio tu kwa meli za mizigo mbali pia za abiria.

Share This Article