Meli kubwa zaidi duniani kutia nanga Mombasa

Tom Mathinji
1 Min Read

Sekta ya utalii humu nchini itafaidika pakubwa huku meli kubwa zaidi duniani ya maktaba MV Logos Hope, ikitarajiwa kutia nanga mjini Mombasa mwezi Agosti.

Meli hiyo itatia nanga miaka 18 baada ya meli ya  Duolos kuzuru taifa hili.

MV Logos itatia nanga katika bandari ya Mbaraki na itafunguliwa kwa umma kuanzia Agosti 23 hadi mwezi Oktoba 3.

Katika mkutano na wanahabari, mwanachama wa kamati andalizi Constanza Figueroa alisema lengo kuu la meli hiyo kutoa habari, usaidizi na matumaini katika kila bandari inayozuru. Hadi kufikia sasa, meli hiyo imetia nanga kwa zaidi ya nchi 150.

“Wageni katika meli hiyo watakuwa na fursa ya kupata zaidi ya vitabu vilivyo na mada zaidi ya 5,000 kwa bei nafuu. Vitabu hivyo ni pamoja na vile vya michezo, sayansi, upishi, sanaa, imani na dawa,” alisema Figueroa.

Aidha, aliwasifu Wakenya kwa ukarimu wao huku akiwahimiza kuonyesha ukarimu huo kwa zaidi ya wahudumu 300 watakaowasili na meli hi hiyo.

Wahudumu watazingatia kutoa mafunzo ya kusoma na kuandika, elimu, ushirikiano wa utamaduni mbalimbali, uhamasisho wa kijamii na kutafakari kuhusu upendo wa Mungu kwa ulimwengu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *