Mchuano wa ligi kuu nchini Ujerumani baina ya Bayern Munich na Union Berlin uliokuwa uchezwe Jumamosi jioni umeahirishwa.
Pambano hilo limeahirishwa kutokana na barafu iliyotanda uwanjani Alienz Arena.
Munich ni ya pili ligini kwa alama 32 kutokana na mechi 12, pointi 2 nyuma ya Bayer Leverkusen.
Barafu hiyo pia imesababisha kufutiliwa mbali kwa safari za ndege kuingia na kutoka mjini Munich.