Mechi mbili za ligi Kuu FKF zafutiliwa uwanjani Kenyatta

Dismas Otuke
0 Min Read

Mechi mbili za Ligi Kuu nchini Kenya FKF zilizoratibiwa kusakatwa Jumapili alasiri katika uwanja wa Kenyatta kaunti ya Machakos, zimefutiliwa mbali kutokana na kulowa maji kwa uwanja huo.

Michuano hiyo ambayo pia ilikuwa iruhswe mubasahara kupitia runing ya KBC ni kati ya Nairobi City Stars dhidi ya Ulinzi Stars na Posta Rangers dhidi ya Talanta FC.

Katika pambano la awali Police FC wamewacharaza Kakamega Homeboyz mabao 2-1.

TAGGED:
Share This Article