Mckinstry ateuliwa kocha mkuu wa Gambia kwa miaka miwili

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama cha soka nchini Gambia kimemteua Mwingereza Jonathan Mckinstry kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Gambia, maarufu kama The Scorpions kwa kandarasi ya miaka miwili.

Hadi uteuzi wa wake Mckinstry aliye na umri wa miaka 38 amewaongoza Gor Mahia kuhifadhi taji ya Ligi Kuu nchini Kenya likiwa kombe la 21 kwa jumla.

Mckinstry ataanza kutekeleza majukumu  ya Juni mosi mwaka huu, huku akitarajiwa  kuwaongoza kwa mechi za kufuzu kwa kombe la Dunia mwaka 2026.

Awali kocha huyo amezinoa timu za taifa za Uganda na Rwanda.

Gambia itawaalika Ushelisheli tarehe 8 mwezi ujao katika mchuano wa kundi F, kabla ya kuzuru Libreville Gabon siku tatu baadaye.

Share This Article