Wing’a wa zamani wa timu za Ushuru FC,AFC Leopards,FC Talanta, Ulinzi Stars, Western Stima na Muhoroni Youth Ezekiel Otuoma ameaga dunia leo akiwa na umri wa miaka 31.
Otuoma amekuwa akiugua ugonjwa wa kuganda kwa neva za mwili.
Mkewe Racheal amethibitisha kifo chake mapema Jumamosi kupitia kwa mtandao wa kijamii.
Otuoma amekuwa akitumia kiti cha magurudumu tangu aanze kulemewa na ugonjwa huo mwaka 2020.
Timu zote alizowahichezea Otuoma zimetoa risala za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii.
Mola ailaze roho yake mahali pema.