Frank Patrick wa umri wa miaka 17, ambaye anafahamika na wengi mitandaoni kama Molingo amefariki.
Kulingana na taarifa, mkazi huyo wa Wilaya ya Chato Mkoani Geita aliaga dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani ambako alikuwa akiuguzwa na mamake mzazi.
Rafiki yake wa karibu ambaye alikuwa akiishi naye na ambaye pia alikuwa akirekodi video za vichekesho vyake aitwaye Mudi Msomali alielezea kwamba Molingo amekuwa akiugua mara kwa mara.
Ugonjwa aliokuwa akiugua hata hivyo haukufahamika lakini kulingana na Msomali, Molingo alikuwa anavimba mwili mzima wakati mwingine na hata kuishiwa damu mwilini.
Alisema kwamba vipimo vya hospitalini havikubaini maradhi hayo lakini walidhania kwamba ni maradhi ya selimundu.
Msomali alisema walishauriwa na madaktari kumrejesha nyumbani ishara kwamba walishaona kafika mwisho lakini wao hawakujua.