Mdhibiti wa bajeti Dkt. Margaret Nyakang’o ,amesema kuwa mchakato wa kuandaa bajeti mpya umekuwa kinyume cha katiba .
Dkt Nyakang’o amesema haya Alhamisi alipofika mbele ya kamati ya bunge inayosimamia utekelezaji wa katiba (CIOC), chini ya uongozi wa Mbunge Gathoni Wamuchomba.
Bi Nyakang’o amehoji hususan kipengee cha 221 kuhusu makisio na makadirio ambayo yanahitajika kuwa na uwazi.
Wamuchomba amekashifu bajeti hiyo akisema ilikuwa na makisio ya matumizi pekee bila makisio ya pato.
Bajeti hiyo pia imekosolewa kwa kuongeza matumizi ya idara ya mahakama ,utumishi wa umma na tume ya kuwaajiri walimu ya TSC, huku idara nyingine zote zikipunguziwa bajeti ya matumizi.