Kocha wa timu ya taifa ya Kenya,Harambee Stars Benni McCarthy, ametaja kikosi cha wanandinga 23 kwa mechi mbili za kufuzu kwa Kombe la Dunia mwezi ujao.
Kikosi cah McCarthy kinawajumuisha wachezaji 13, walioshiriki fainali za kombe la CHAN mwaka huu.
Mshambulizi chipukizi Job Ochieng anayepiga soka ya kulipwa katika klabu ya Real Sociadad B nchini Uhispania, ameitwa kikosini kwa mwara ya kwanza.
Harembee Stars itawaalika Gambia tarehe 5 mwezi ujao katika uwanja wa Kasarani katika mchuano wa kundi F, kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao kabla ya kupimana nguvu na Ushelisheli tarehe 9 katika uo huo wa Kasarani.
Kenya ni ya nne katika kundi F kwa pointi 6 ,pointi 9 nyuma ya viongozi Ivory Coast.